KONDOMU - PowerPoint PPT Presentation

1 / 20
About This Presentation
Title:

KONDOMU

Description:

... wa kwanza unarudi kwa ... wa uhakiki, majiribio ya kwanza ya kondomu, kwa elekroniki ... kuu ya pili ya dunia, veterani walilete kondomu za kwanza nchini. ... – PowerPoint PPT presentation

Number of Views:354
Avg rating:3.0/5.0
Slides: 21
Provided by: tgps
Category:
Tags: kondomu | kwanza

less

Transcript and Presenter's Notes

Title: KONDOMU


1
KONDOMU
Vitini hivi vimetayarishwa na TGPSH/GTZ na
PSI-Tanzania.
2
Historia ya Kondomu
  • Imetayarishwa kwa ushirikiano baina ya TGPSH/GTZ
    na PSI-Tanzania

3
Kondomu ni nini?
  • Kondomu
  • Ni kama mfuko uliotengenezwa kwa kutumia
    mpira,plastiki au ngozi za wanyama
  • Inahifadhi mbegu za kiume kabla, wakati na baada
    ya mwanaume kukojoa
  • Ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango na pia ni
    kinga dhidi ya kuzuia magonjwa ya zinaa pamoja na
    virusi vya Ukimwi (VVU)
  • huepusha uume kuguswa na maji maji yatokayo
    ukeni.

4
Historia ya Kondomu..
  • Kondom zinaweza kufuatiliwa takribani miaka elfu
    iliyopita
  • Ushahidi wa kwanza unarudi kwa Wamisri!!
  • Katika miaka ya 1000 KK, walitumia mpira laini
    kujikinga kutokana na magonjwa ya zinaa

5
Na wapi tena kwingine?
  • Michoro ya mapangoni iliyopo cambarelles nchini
    Ufaransa inaonyesha kuwa katika kipindi cha
    miaka ya 100-200 BK kulikuwa na matumizi ya
    kondomu.

6
Malighafi gani ilitumika kutengeneza kondomu?
  • Kondomu hizi zilitengezwa kwa malighafi isiyo
    kawaida
  • Mafuta ya hariri
  • Karatasi
  • Tumbo la samaki
  • Gamba la kobe

7
Mabadiliko ya kondomu
  • Kuna kipindi kondomu zilifungwa na kamba
    nyembamba..

8
Zatumiwa kama kinga dhidi ya maradhi
  • - miaka ya 1500
  • Janga la Kaswende lasambaa Ulaya
  • Muitaliano, Gabrielle Fallopius, anajitangaza
    kutengeza kondomu ili kuwakinga wanaume kutokana
    na ugonjwa huo
  • Alifanya majaribio miongoni mwa wanaume 1,100
    kutumia kondomu, hakuna anayeambukizwa kaswende.

9
Mabadiliko ya kondomu
  • Baadaye katika miaka ya 1500.. ufanisi wa
    matumizi ya kondomu katika kuzuia mimba
    unagundulika.
  • Kondomu zinarekebishwa
  • Mifuko ya kitambaa ililowekwa kwenye kemikali na
    kuruhusiwa kukauka kabla ya matumizi.
  • Zilikuwa kondomu za kwanza zenye kemikali ya kuua
    mbegu za kiume.

10
Mabadiliko ya kondomu
  • Katika miaka ya 1700, uwenzo wa kondomu katika
    uzazi wa mpango unaanza kufahamika.
  • Kondomu zinazotengenezwa kwa utumbo wa wanyama
    zinaanza kuwepo.
  • Kondomu za aina hii zinajulikana na kuongezeka
    umaarufu.

11
Mabadiliko ya kondomu
  • Miaka ya 1800,
  • Utengenezaji wa kondomu unabadilika baaada ya
    kugundulika maarifa ya kuchemsha malighafi ya
    mpira na sulphur ili kuifanya iwe mpira imara na
    unaonyumbulika.
  • Hii iliwezesha kutengeneza bidhaa za mpira
    zikiwamo kondomu, haraka na kwa bei nafuu.
  • Matokeo yake,matumizi ya kondomu yanaongezeka

12
Kondomu ya mpira
13
Mabadiliko ya kondomu
  • Miaka ya 1900
  • Mpaka mapema miaka ya 1900
  • kondomu nyingi zilitengenezwa kwa kuchovya
    mikono kwenye mchanyato wa mpira.
  • ubora wake haukuwa thabiti

14
Mabadiliko ya kondomu
  • Mwaka 1919,
  • Fredrick Killian alianzisha uchovyaji kwenye
    mpira laini.
  • Kondomu za mpira zilikuwa bora kwani zilidumu kwa
    muda mrefu zaidi, nyembamba na hazikuwa na
    harufu.

15
Ona mabadiliko??
16
Historia ya Kondomu
  • Katikati ya miaka ya 1930, watengenezaji wakubwa
    nchini Marekani walikuwa wakitengeneza kondomu
    milioni 1.5 kwa siku.
  • 1950 Ubora wa uhakiki, majiribio ya kwanza ya
    kondomu, kwa elekroniki yaanza.
  • Mwaka 1957, kondomu ya kwanza yenye kilainishi
    yazinduliwa Uingereza.

17
Historia ya Kondomu
  • Mwaka 1974 Dawa ya kuua mbegu za kiume ilianza
    kuwekwa kwenye kondomu.
  • Mwaka1994 kondomu za kiume zilizotengenezwa kwa
    plastiki (polyurethane) ziliingizwa kwenye soko.

18
Historia ya kondomu Tanzania
  • Baada ya vita kuu ya pili ya dunia, veterani
    walilete kondomu za kwanza nchini.
  • Mwanzo wa miaka ya 70,kondomu zililetwa kwa ajili
    ya kupanga uzazi na UMATI.
  • Utumiaji uliongezeka miaka ya 1980 baada ya janga
    la UKIMWI.

19
KONDOMU ZINAZOPATIKANA TANZANIA.
  • Kondomu za kiume zinazopatikana Tanzania
    zinatengenezwa kutokana na mpira laini.
  • Kondomu za kike zinazopatikana (kiasi kidogo)
    zinatengezwa na malighafi ya plastiki.

20
Usambazaji wa kondomu Tanzania
  • Mwaka 2003,
  • Jumla ya kondomu 48.5 milioni zilisambazwa na
    mtandao wa vyombo vya kibiashara na kijamii
Write a Comment
User Comments (0)
About PowerShow.com