Title: SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2002
1SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2002
2 JUMLA YA WAKAZI TANZANIA BARA
- WANAUME 16,427,702
- WANAWAKE 17,156,905
- JUMLA KUU 33,584,607
3JUMLA YA WAKAZI TANZANIA VISIWANI
- WANAUME 482,619
- WANAWAKE 502,006
- JUMLA KUU 984,625
4JUMLA YA WAKAZI TANZANIA
- WANAUME 16,910,321
- WANAWAKE 17,658,911
- JUMLA KUU 34,568,232
5IDADI YA WATU ( Millioni)
6KASI YA ONGEZEKO LA WATU, TANZANIA BARA
- Kasi ya ongezeko la watu kati ya mwaka 1988
2002 ni asilimia 2.9 kwa mwaka
7KASI YA ONGEZEKO LA WATU, TANZANIA VISIWANI
- Kasi ya ongezeko la watu kati ya mwaka 1988
2002 ni asilimia 3.1 kwa mwaka
8KASI YA ONGEZEKO LA WATU, TANZANIA
- Kasi ya ongezeko la watu kati ya mwaka 1988
2002 ni asilimia 2.9 kwa mwaka
9Wastani wa Kasi ya Ongezeko ya Watu
10 Wastani wa Kasi ya Ongezeko la Watu Kimkoa
- Kasi ya ongezeko ya watu ni tofauti mkoa hadi
mkoa - Kasi ya ongezeko ni kubwa kwa mkoa wa Kigoma
(4.8)
11 Wastani wa Kasi ya Ongezeko la Watu Mikoani
- Kiwango cha chini kipo Lindi (1.4)
12 Wastani wa Kasi ya Ongezeko la Watu Katika
Miji Mikubwa
- Vile vile kasi ni kubwa katika miji ya
- Dar es Salaam (4.3)
- Mjini Magharibi (4.5)
13IDADI YA KAYA
- IDADI YA KAYA, TANZANIA BARA 6,811,087
- IDADI YA KAYA, TANZANIA VISIWANI 184,949
14IDADI YA KAYA
- JUMLA YA KAYA TANZANIA 6,996,036
-
- WASTANI WA UKUBWA WA KAYA 4.9
15MSONGAMANO WA WATU
- Msongamano wa watu Tanzania Bara ni watu 38 kwa
kila kilomita moja ya mraba - Msongamano wa watu Tanzania Visiwani ni watu 398
kwa kila kilomita moja ya mraba - Msongamano wa watu Tanzania ni watu 39 kwa kila
kilomita moja ya mraba
16MSONGAMANO WA WATU KIMKOA
- Msongamano wa watu ni tofauti mkoa hadi mkoa
- Msongamano wa watu kwa mikoa ya zanzibar kwa
ujumla ni mkubwa ( 111 mpaka 1700)
17MSONGAMANO WA WATU KIMKOA
- Kwa Tanzania Bara mikoa iliyo na msongamano
mkubwa ni - Dar es Salaam (1793), Mwanza (150)
- Kilimanjaro (104)
18 MSONGAMANO WA WATU KIMKOA
- Mikoa iliyo na msongamano mdogo ni mikoa ya
Ruvuma (18), Rukwa (17) na Lindi(12)
19UWIANO KATI YA WANAWAKE NA WANAUME
- Kila kundi la wanawake 100 kuna wanaume 96 kwa
Tanzania
20UWIANO KATI YA WANAWAKE NA WANAUME KIMKOA
- Mikoa ya Dar es Salaam (102), Manyara (106),
kuna wanaume wengi zaidi kuliko wanawake - Unguja Kusini(103) kuna wanaume wengi zaidi
kuliko wanawake
21 UWIANO KATI YA WANAWAKE NA WANAUME KIMKOA
- Kwa mikoa mingine iliyobaki wanawake ni wengi
zaidi kuliko wanaume
22TAKWIMU NYINGINE
- Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kutoa
takwimu nyingine kila baada zitakapokuwa tayari - Ofisi inategemea kuchapisha muhtasari wa takwimu
za kitaifa, kimikoa na kiwilaya.
23TAKWIMU NYINGINE
- Takwimu nyingine zitatolewa kwa njia ya
(electronic format) (diskettes), kwa watumiaji
wa takwimu (data users) - Kuwekwa kwenye Website ya Taifa iliyo chini ya
Ofisi Rais, Mipango na Ubinafsishaji
24TAKWIMU NYINGINE
- Ofisi ya Taifa ya Takwimu inayo mpango wa
kupunguza gharama za Serikali za uchapishaji wa
vitabu wa takwimu zake. Website ya Taifa
itatumika kwa ajili ya (dissemination) katika
wilaya zote. - CD-ROM zitatumika pia
25VITABU VITAKAVYOCHAPISHWA
- Kitabu cha awali chenye taarifa ya jumla ya watu
wote, kitaifa, kimkoa, kiwilaya na kikata /
Shehia kwa jinsia zao, kasi ya ongezeko la watu
tangu mwaka 1988, uwiano wa wanawake na wanaume
n.k. Kitabu hiki kilitoka mwezi Februari 2003.
26VITABU VITAKAVYOCHAPISHWA
- Vitabu vya Wilaya Zote (District Profiles)-
Taarifa zitakazokuwepo kwenye vitabu hivi ni
mchanganua wa hali ya watu kiumri, kijinsia, hali
ya elimu, uchumi, vizazi, vifo, hali ya makazi,
ulemavu, etc. - Vitabu vya Mikoa yote (Regional Profile)
Taarifa za vitabu hivi ni sawa na za wilaya
isipokuwa zitatolewa kimkoa
27VITABU VITAKAVYOCHAPISHWA
- Vitabu vya Vijiji ( Village Statistics
Booklets) Kila wilaya itakuwa na kitabu chake
kitakachoonyesha idadi ya wakazi kijinsia, kiumri
na hali ya ndoa kwa vijiji vyote.
28VITABU VITAKAVYOCHAPISHWA
- Kitabu cha hali ya uzazi na vifo (Fertility and
Mortality Statistics). Kitabu hiki kitachanganua
hali ya vifo na uzazi kiwilaya, kimkoa na kitaifa.
29Kitabu cha Makisio ya Watu (Population
Projections Booklet)
- Kitabu kitakuwa na makisio ya wakazi wote
Tanzania kuanzia mwaka 2003 mpaka 2011 wakati
tutakapokuwa tunangoja sensa nyingine tena
ifanyike. - Kitabu hiki kitakuwa na takwimu za kiwilaya,
kimkoa na kitaifa kwa upande wa kijiji na kimji.
30Takwimu za Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2002
- Viongozi wote wa nchi, Waheshimiwa Wabunge,
Mabibi na Mabwana, tutumie takwimu hizi
zilizokusanywa kitaalamu kwa ajili ya kupanga
mipango sahihi ya maendeleo ya taifa letu.
31TAKWIMU SAHIHI KWA AJILI YA MIPANGO MAKINI