About This Presentation
Title:

Description:

Uongozi wa SACCOS uendelee kusimamia majengo hadi hapo Hisa zote za Kismati zitakaponunuliwa na wanachama mmoja mmoja. – PowerPoint PPT presentation

Number of Views:3
Avg rating:3.0/5.0
Slides: 29
Provided by: user3254

less

Transcript and Presenter's Notes

Title:


1
UMILIKISHAJI WA MAJENGO YA CHAMA KWA WANACHAMA
KATIKA SEMINA YA WANACHAMA TAWI LA DSMUKUMBI
WA IPP HALL DSM21.9.2013- 22.9.2013
  • By Henry J. Bwogi Jasson C. Kalile
  • Wajumbe wa Bodi ya Posta na Simu SACCOS Ltd

2
Sehemu sita za mada
  • Utangulizi
  • Majengo ya SACCOS
  • Umilikishaji Majengo kwa Wanachama
  • Manufaa na athari Majengo kuwa Mali ya wanachama
  • Mapendekezo
  • Hitimisho

3
UTANGULIZI
  • Lengo la Wasilisho
  • Kuwapa Wanachama taarifa/uelewa juu ya
    Umilikishwaji wa Majengo ya chama
  • Kufuatia Azimio la Mkutano Mkuu wa mwaka 1996
    ambapo Wanachama waliazimia kuendeleza Chama kwa
    kusamehe kuchukua magawio yao katika Chama.
  • Wanachama walikusudia fedha watakazosamehe
    zitumike kujenga majengo kama kitega uchumi.

4
Utangulizi
  • Baada ya wanachama kusamehe magawio ya mwaka
    1997, 1999, 2001, 2003 na 2005 majengo mawili
    yalijengwa
  • Majengo yalimilikiwa na SACCOS
  • Wanachama waliosamehe magawio yao walitaka
    wamilikishwe majengo hayo.

5
Majengo ya SACCOS
  • Majengo haya yalikuwa mali za Chama.
  • Yalitumika kama dhamana wakati chama kinakopa
    katika taasisi za fedha.
  • Wana Ushirika tunasema Nguvu ya mnyonge ni
    umoja.
  • Wanachama wote walinufaika na majengo haya.

6
Umilikishaji Majengo
  • Wanachama waliochangia ujenzi wa majengo hayo
    wanaona nguvu zao zinapotea bure.
  • Hivyo wazo la kuwamilikisha likaanza kujitokeza.
  • BODI ilianza mchakato wa taratibu za umilikishaji
    wa Majengo kwa Wanachama kama walivyochangia.

7
Kanuni za ukokotoaji
  • Kanuni ya kukokotoa gawio ilikuwa kwa Akiba
    (Bonus) 1997- 2001
  • Kanuni ya kukokotoa gawio ilikuwa kwa Hisa
    (Gawio) 2003- 2005.

8
Umilikishaji Majengo..
  • Idadi ya wanachama waliosamehe magawio na kiasi
    cha fedha
  • Mwaka 1997- 6,424 Sh. 123,155,186
  • Mwaka 1999- 5,401 Sh. 227,115,629
  • Mwaka 2001- 5,140 Sh. 423,337,220
  • Mwaka 2003- 5,010 Sh. 276,166,618
  • Mwaka 2005- 4,941 Sh. 242,815,538
  • Jumla Sh. 1,292,590,191

9
Ujenzi wa Majengo
  • Ujenzi ulianza Septemba, 2001 kwa azimio la
    Mkutano Mkuu wa 25.8.2001 na kukamilika Septemba
    2003
  • Jengo la Ofisi liligharimu Sh 1,984,226,902
  • Jengo la Kuegesha magari lilianza kujengwa 2005
    na kukamilika 2008
  • Jengo la kuegesha magari liligharimu Sh
    2,899,288,530

10
Mapato ya Majengo
Mwaka Mapato Matumizi Ziada
2004 38,569,527 12,784,677 25,784,851
2005 109,895,939 12,045,957 97,849,982
2006 104,873,260 11,670,360 93,202,901
2007 66,148,930 50,403,871 15,745,059
2008 105,544,313 87,905,036 17,639,277
2009 131,396,685 55,274,739 76,121,946
2010 137,241,629 56,041,499 81,200,130
2011 151,058,537 75,220,603 75,837,933
Jumla 844,728,820 361,346,742 483,382,079
11
Vigezo vya Uthaminishaji
  • Ili kupata thamani ya Hisa katika jengo lazima
    ujue Thamani ya Mali (Majengo) yatakayogawiwa
    Hisa. Vigezo vifuatavyo vilitumika
  • Mapato
  • Hali ya Soko

12
Kigezo Mapato ya jengo
  • Kigezo cha Mapato kimetumika kupata thamani ya
    hisa kutokana na kuwa na mtiririko mzuri wa
    mapato kwa miaka 8 (2004- 2011)
  • Pia kwa kukadiria mwelekeo wa mtiririko wa Mapato
    kipindi kijacho
  • Hata, hivyo utawala na uongozi mbovu wa mali hii
    unaweza kufanya hasara inayoweza kuwagharimu
    wenye mali
  • Gharama kubwa zisipodhibitiwa zinaweza kuondoa
    ndoto ya uzuri na Thamani ya Majengo
  • Hivyo, Uzuri tunao uona unapaswa kusimamiwa
    ipasavyo

13
Kigezo Hali ya Soko
  • Kigezo hiki hutaka kulinganisha Mali zinazofanana
    zilizopo sokoni na au zilizouzwa na thamani yake
  • Ukitaka kujua thamani ya kitu kipoteze .
  • Tatizo hapakuwa na majengo kama haya yaliyouzwa.
  • Pia ilikuwa vigumu kulinganisha majengo yaliyo
    sehemu tofauti (Kkoo, Manzese, Msasani nk)
  • Ni vigumu kubashiri ukuaji wa mji kwa miaka ijayo
    kama hautaathiri thamani ya mali (Kigamboni)

14
Uthaminishaji
  • Baada ya kuona ugumu katika vigezo vya Mapato na
    Soko, Utaratibu mchanganyiko wa kimahesabu
    ulitumika pamoja na Mapato na hali ya soko
  • Discount Principle Pata thamani ya mali kwa siku
    zijazo ukilinganisha na sasa.
  • Net Present Value Kiasi/(1i) Hii huonesha
    thamani ya fedha za siku zijazo sasa.
  • Discount Factor 1/(1r)t
  • BAADA YA UKOKOTOAJI -
  • Hisa moja itakuwa Sh. 3,750/
  • Mwanachama atamiliki hisa zisizopungua 90 zenye
    thamani ya Sh. 337,500

15
Mchanganuo wa HISA
  • Jumla ya hisa 1,195,300 zenye thamani ya Tshs.
    4,482,375,000/ ambazo ziko katika makundi makuu
    matatu
  • Hisa za Wanachama mmoja mmoja 597,650 zenye
    thamani ya Tshs. 2,241,187,500/
  • Hisa za Chama 358,590 zenye thamani ya Tshs.
    1,344,712,500/
  • Hisa za Kismati 239,060 zenye thamani ya Tshs.
    896,475,000

16
Wamiliki halali wa Majengo
  • Waliosamehe magawio kuanzia 1997 hadi 2005,
  • Gawio la mwisho la 2005 lilichukuliwa na chama
    mwaka 2007
  • Siku ya mwisho ya hesabu za mwaka 2007 ni tarehe
    31.12.2007
  • Hii ni siku inayotenganisha wamiliki na wasio
    wamiliki. (Cut- off date)
  • Hivyo wote waliosamehe magawio ni wamiliki halali
  • Wanachama walioingia chama mwaka 2006 na baada ya
    hapo watatakiwa kununua hisa iwapo watahitaji.
  • Na wale wanachama wenye hisa pungufu ya hisa 90
    watatakiwa kuongeza .

17
Manufaa na Athari za Kumiliki Majengo
  • Faida Kiuchumi
  • Kukwepa mfumuko wa bei
  • Kupata gawio kila mwaka majengo yanapopata faida
  • Huvutia ukodishaji (upangishaji)
  • Faida Kijamii
  • Mwanachama kuthaminiwa na jamii kutokana na
    kumiliki mali
  • Kuwa na mamlaka zaidi na mali yake
  • Anaweza kurithisha umiliki wake

18
Faida na hasara
  • Faida kwa ujumla
  • Kupanga viwango vya upangishaji
  • Inampa uwezo wa kuwa mwekezaji na kupata faida ya
    uwekezaji
  • Ni Mali inayoshikika (Tangible)
  • Uwezo wa kushawishi mafanikio (kuboresha majengo,
    kuwa na wapangaji wenye uwezo kifedha, kuongeza
    mali nyingine nk)

19
Faida na hasara
  • Hasara
  • Udhibiti mdogo
  • Kushuka kwa mapato hupunguza gawio na hivyo
    kushusha thamani ya hisa
  • Hisa zikinunuliwa kutoka kwa mwekezaji na kurudi
    chamani thamani yake huwa chini (ndogo)
  • Mgawanyiko ndani ya chama walionacho na
    wasiokuwa nacho (Utengano ni UDHAIFU)

20
Faida na hasara
  • Hasara
  • Kodi italipwa Serikalini
  • Urejeshaji wa gharama za ujenzi kuchukua muda
    (miaka) mrefu
  • Uwekezaji usiotabirika katika mabadiliko ya soko
  • Sheria na Kanuni
  • Wapangaji kuhama jengo (wazi)
  • Uchelewesho wa malipo ya pango

21
Faida na hasara
  • Hasara
  • Gharama kubwa za matengenezo, ukarabati na
    Uchakavu
  • Bima
  • Majanga (Kimbunga, Tetemeko la Ardhi, Kuvunjwa na
    wezi nk)
  • Kukinyima chama uwezo wa kutumia majengo kama
    dhamana ya Mikopo.

22
Mapendekezo
  • Wanachama wote waliosamehe magawio wapewe Hisa za
    moja kwa moja (Automatic)
  • Mwanachama atatakiwa kuwa na Hisa zisizopungua 90
    za thamani ya Sh 337,500
  • Umiliki wa hisa utakuwa kwa uwiano wa 352
    (Chama MwanachamaKismati)
  • Hisa za Kismati (Goodwill) zitauzwa kwanza. Hivyo
    atakayetaka kununua Hisa anunue hizo kwanza
  • Hisa za Kismati zikiisha mwanachama atanunua hisa
    kutoka kwa mwanachama anayeuza.
  • Chama hakitanunua hisa kutoka kwa mwanachama

23
Mapendekezo
  • Mwanachama aliye na Hisa kwenye majengo lazima
    awe mwanachama wa SACCOS
  • Mwanachama anayetaka kununua Hisa za Majengo
    lazima awe mwanachama wa SACCOS kwanza (DUAL
    membership)
  • Mwanachama aliyeacha uanachama lakini alisamehe
    magawio, uanachama wake katika majengo utakuwa
    DOMANT hadi atakapo uhuisha

24
Mapendekezo
  • Endapo hatahuisha uanachama wake ndani ya mwaka
    mmoja tangu Azimio la Mkutano Mkuu wa Baraza la
    Wawakilishi hisa zake zitarudishwa kwenye Hisa za
    KISMAT(Goodwill) kwa ajili ya kuuzwa
  • Mwanachama akifariki, mrithi wake anaweza
    kuendeleza uanachama.
  • Kila mwana hisa atapatiwa Hati ya HISA
    inayoonesha idadi ya Hisa anazomiliki katika
    majengo

25
Mapendekezo
  • Uongozi wa SACCOS uendelee kusimamia majengo hadi
    hapo Hisa zote za Kismati zitakaponunuliwa na
    wanachama mmoja mmoja.
  • SACCOS iandae daftari la wanahisa wa majengo na
    hisa zao na kulisambaza nchi nzima (matawini)
  • Uendelezaji wowote mpya wa mali na viwanja vya
    SACCOS usihusishwe katika ripoti hii.

26
HITIMISHO
  • Maazimio ya Mwaka 1996 yamekuwa chachu kubwa ya
    Maendeleo makubwa ndani ya Posta na Simu SACCOS.
  • Wanachama walitoa maamuzi mazito bila kujali
    athari Risk taking
  • Sasa kila aliyesamehe gawio amepewa Hisa
    kulingana na alivyochangia.
  • Mchango wa kila mmoja una thamani kubwa
  • Kila Hisa itauzwa TZS 3,750 (Minimum Hisa 90 kwa
    kila mwanachama)

27
Hitimisho
  • Mwanachama mwenye kutaka kumiliki Majengo lazima
    awe mwanachama hai wa SACCOS
  • Mwanachama anayetaka kuuza Hisa lazima asubiri
    hadi Hisa za Kismati ziishe
  • Heko wanachama kwa kufanya maamuzi haya muhimu
    kwenu na kwa kizazi kijacho

28
Mwisho
  • Tunawashukuru sana kwa kutusikiliza
  • Asanteni sana
Write a Comment
User Comments (0)